Sunday, April 3, 2011

DADA MWINGINE WA KIKOMBE AIBUKA MOROGORO


Vikombe vikiwa vimejazwa  dawa inayodaiwa kutibu magonjwa mbalimbali sugu inayotolewa na Dada Fatma Said Senga ( 41) mkazi wa Kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro, ambapo watu zaidi ya 200 wamepata kikombe hicho ambapo gharama ni shilingi za kitanzania 200 tu.
Dada Fatma Said Senga akiwa na mjukuu wake Ashinuli Ally Pitchuo ( 4) ambaye ni mgawaji wa dawa yake kwa wagonjwa na kulia ni mmoja wa ndugu yake anayeishi nae nyumbani hapo
Dada Fatma Said Senga akiwaonesha viongozi waliomtembelea nyumbani kwake eneo la Kichangani, Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kupata maelezo ya kina kuhusu tiba yake hiyo ( anaye mfuatia ) ni mwandishi wa habari aliyetembelea eneo
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu ( kulia) akimpatia maelekezo ya Dada Fatma Said Senga anayewatibia ya watu wenye magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu kikombe cha dawa aweze kusajili huduma hiyo na kupimwa dawa yake ili kulinda usalama wa afya ya watumiaji

Dada Fatma Said Senga ( 41) mkazi wa Kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro, ( mwenye ushungi mwekundu ) akimwaonesha viongozi waliomtembelea nyumbani kwake eneo la Kichangani, Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kupata maelezo ya kina kuhusu tiba yake hiyo ( anaye mfuatia ) ni mwandishi wa habari aliyetembelea eneo hilo Machi 31, mwaka huu wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu ( hayupo pichani), kazi hiyo ameianza machi 30, mwaka huu na kikombe ni ‘bati’ (sh. 200/-). Picha zote na John Nditi, Morogoro .
VN:F [1.9.7_1111]

No comments:

Post a Comment